Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waitaka Iraq kubaini chanzo cha mashambulizi

UM waitaka Iraq kubaini chanzo cha mashambulizi

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq ametoa mwito akitaka serikali ya taifa hilo kusaka njia mjarabu itayobainisha chanzo cha kujiri matukio ya mashambulizi ya mara kwa mara.

Pamoja na kuelezea masikitiko yake kutokana na mashmbulizi hayo, Martin Kobler amesema serikali inapaswa kujua chanzo cha kujirudia rudia kwa hali hiyo ambayo amesema kuwa inazorotesha ustawi wa taifa hilo.

Amesema ni nivigumu kuona mamia ya watu wakiendelea kupoteza maisha huku serikali ikisalia kukaa kimya bila kubainisha chanzo cha mauwaji hayo.

Kwa mujibu wa taarifa toka duru mbalimbali za habari, kumeshuhudia milipuko kadhaa katika maeneo mbalimbali ya taifa hilo na kuuwawa madarzeni ya watu huku wengine wakijeruhiwa vibaya.