Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Michezo ni muhimu kwa amani na maendeleo:Lemke

Michezo ni muhimu kwa amani na maendeleo:Lemke

Mshauri wa katibu mkuu wa Umoja wa Umoja wa Mataifa kuhusu umuhimu wa michezo kwenye mandeleo na amani Wilfried Lemke yuko mjini Berlin Ujerumani ambapo amehutubia kikundi cha kamati ya michezo cha bunge la Ujerumani kuhusu sera za kimataifa za michezo ambapo aliangazia shughuli zake kwa muda wa mwaka mmoja uliopita.

Mwishoni mwa juma bwana Lemke alipata fursa ya kubadilishana mawazo na baadhi ya wanachama wa bunge la Ujerumani pamoja na msimamizi wa Umoja wa Mataifa mjini Geneva bwana Clemens Adams na mwakilishi wa kudumu kutoka Ujerumani kwenye Umoja wa Mataifa mjini Geneva balozi Hanns Heinrich Schumacher, mkutano uliowavutia wabunge wengi kutoka Ujerumani.

Ijumaa iliyopita bwana Lemke alisafiri kwenda Poland ambapo alishiriki kwenye uzinduzi wa programu ya kupinga ubaguzi ya mwaka 2012 ya kombe la Ulaya UEFA.