Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ICT ni muhimu kwa mustakhbali tunaoutaka:ITU

ICT ni muhimu kwa mustakhbali tunaoutaka:ITU

Muungano wa wa teknolojia ya mawasiliano ITU umesema katika mktano wa Rio+20 unasisitiza kwamba teknolojia ya habari na mwasiliano ICT ni kiungo muhimu katika kupiga hatua na kutokomeza umasikini, hivyo ni lazima itamblike kama muundombinu muhimu unaoweza kuunganisha masuala ya kijamii na kuleta maendeleo endelevu.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa ITU Hamadoun Toure teknolojia ya habari na mawasiliano lazima ipewe kipambele katika matokeo na muafaka utakaoafikiwa kwenye mkutano wa Rio+20.

Toure ameongeza kuwa tekinolojia ya habari na mawasiliano ina athari kwa nguzo zote tatu za maendeleo endelevu ambazo ni ukuaji wa uchumi, majmuisho ya kijamii na kulinda mazingira.