Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matumizi bora ya nishati muhimu kwa chakula:FAO

Matumizi bora ya nishati muhimu kwa chakula:FAO

Kilimo kinachotegemea zaidi nishati za kisukuku kinapunguza uwezo wa sekta hiyo kuzalisha chakula cha kutosha, na hivyo kuongeza umaskini na kudhoofisha juhudi za kuweka uchumi endelevu kote ulimwenguni, limesema shirika la kilimo na chakula, FAO.

Onyo hili limetolewa katika ripoti ya shirika hilo la Umoja wa Mataifa kufuatia utafiti kuhusu uzalishaji chakula wenye kutumia nishati vizuri, kabla ya mkutano wa kimataifa kuhusu maendeleo endelevu wa Rio+20, ambako changamoto za matumizi ya nishati duniani zitapewa kipaumbele. George Njogopa anaripoti

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)