Msaada na uwekezaji ni muhimu kwa demokrasia Myanmar:Suu Kyi

Msaada na uwekezaji ni muhimu kwa demokrasia Myanmar:Suu Kyi

Kiongozo anayeunga mkono masuala ya demokrasia nchini Myanmar Aung San Suu Kyin amesema kuendeleza mchakato wa mabadiliko nchini humo ni jukumu la pamoja la watu wa Myanmar, serikali, viongozi wa siasa na jeshi.

Akizungumza mjini Geneva Bi Suu Kyi amesema hata chuki yoyote dhidi ya utawala wa kijeshi yaani Junta uliomuweka katika kifungo cha nyumbani kwa zaidi ya miaka 22.

Ameongeza kuwa hadhi ya jeshi na heshima yake inatokana na jinsi inavyowalinda na kuwatetea watu badala ya kuwatawala. Bi Suu Kyi amesema uhalifu wa zamani nchini Myanmar lazima ushughulikiwe lakini kwa njia ambayo inachagiza maridhiano na sio adhabu.

Ametaja kuwa kuheshimu utawala wa sheria ni suala muhimu katika kumaliza migogoro ya kikabila ambayo inaendelea katika sehemu za Magharibi mwa Myanmar.

(SAUTI YA ANG SANG SUU KYI)