Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban atunukiwa tuzo ya amani ya Seoul Korea

Ban atunukiwa tuzo ya amani ya Seoul Korea

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea kuwa ni kama mtu aliyepewa “heshima ya hali ya juu” kutokana na tuzo la amani lililotolewa kwake.

Ban ametunikiwa tuzo linalojulikana Seoul Peace ambayo imetokana na kutambua mchango wake mkuu kwenye chombo cha Umoja wa Mataifa .

Kamati ya uteuzi ilitangaza hapo jumanne kuwa ametunukiwa tuzo hilo kutokana na mchango wake mkubwa wa kupigania na kutetea haki za kina mama na watoto, kukabiliana na changamoto za umaskini katika nchi zinazoendelea na uchangiaji wa ujenzi wa demokrasia katika nchi za mashariki ya kati.

Tuzo hilo la amani la Seoul lilianzishwa mwaka 1990 kama sehemu ya kumbukumbu ya michuano ya Olympic iliyofanyika mjini Seoul na kufanikiwa kwa kiwango kikubwa.