Mcheza filamu Geena Davis ateuliwa mjumbe maaalum kwenye kampeni ya kutoa hamasisho kuhusu umuhimu wa teknolojia ya mawasiliano miongoni mwa akina mama na wasichana
Shirika la mawasiliono la Umoja wa Mataifa limemteua mcheza filamu maarufu Geena Davis kama mjumbe wake maalum kwenye hamasisho kuhusu mchango unaoweza kutolewa na teknolojia kwenye maisha ya akina mama na wasichana.
Moja ya wajibu wake utakuwa kuongoza kampeni yenye kichwa “Teknolojia inahitajia wasichana”,kampeni ambayo itachukua miaka mitatu ikiwa na lengo la kutoa hamasisho kuhusu jinsi habari na teknolojia za mawasiliano zinaweza kuwainua wanawake.
Davis amesema kuwa ni jambo muhimu kuwawesesha wanawake na wasichan na kuungana na mawasiliano ya teknolojia akiongeza kuwa atakayefanikisha ndoto hii ni chama cha teknolojia cha kimataifa ITU.