Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

EU yatakiwa kushirikiana na Tunisia kuboresha haki za wahamiaji

EU yatakiwa kushirikiana na Tunisia kuboresha haki za wahamiaji

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za wahamiaji Francois Crepeau ameitaka jumuiya ya ulaya kubuni mpango wa uhamiaji ambao utahakikisa kuwa haki za wahamiaji zinaheshimiwa na kulindwa.

Mjumbe huyo amezitaka serikali za bara Ulaya kubuni sheria na kuwa na ushirikiano na Tunisia ushirikiano ambao utakuwa kando na masuala ya usalama kwa lengo la kuboresha haki za wahamiaji.

Mjumbe huyo alikuwa nchini Tunisia kati ya tarehe 3-8 mwezi huu ikiwa ni sehemu ya utafiti ambao utamchukua mwaka mmoja kuhusu mipaka ya mataifa ya Ulaya shughuli ambayo itampeleka kwenye nchi wanakopitia wahamiaji na pia wanazotumia kuingia Ulaya.