Ban asihi kila nchi kutimiza wajibu wake kupiga vita UKIMWI

11 Juni 2012

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, ametoa wito kwa kila taifa kote ulimwenguni kutimiza wajibu wake katika kuhakikisha kuwa watoto hawaambukizwi virusi vya UKIMWI na wanawake wazazi hawafariki kutokana na UKIMWI.

Amesema wanawake na watoto wanafaa kuzingatiwa kwa njia maalum katika vita hivi. Ameyasihi mataifa kuongeza kasi na juhudi, kwa kuunga mkono mpango wa kimataifa wa kukomesha kabisa maambukizi miongoni mwa watoto ifikapo mwaka 2015, na kuhakikisha akina mama hawafariki.

Pia ameelezea umuhimu wa kukomesha kabisa unyanyapaa, akisema kuwa unakuwa kizuizi katika kufikia lengo kuu.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter