Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano kuhusu mpango wa nyuklia nchini Iran wakosa kuzaa matunda

Mkutano kuhusu mpango wa nyuklia nchini Iran wakosa kuzaa matunda

Shirika la Umoja wa Mataifa la kudhibiti nishati ya nyuklia IAEA limesema kuwa hakuna hatua zozote zilizopigwa wakati wa mkutano na maafisa kutoka Iran mwishoni mwa juma jinsi ya kutatua mzozo kuhusu mpango wa nyuklia nchini Iran.

Maafisa wa ngazi za juu kutoka IAEA walikutana na ujumbe kutoka Iran mjini Vienna yaliyo makao makuu ya shirika hilo kukubaliana kuhusu njia za kutafuta suluhu la mzozo wa mpango wa nyuklia nchini Iran.

IAEA inasema kuwa hakuna hatua zilizopigwa kuwa Iran iliibua masuala ambayo tayari yamekwisha zungumziwa na kuongeza mengine mapya. Mataifa kadha yanautaja mpango wa nyuklia kuwa wa kijeshi huku Iran ikishikilia kuwa mpango wake ni wa amani.