Singapore yaridhia mkataba wa ILO wa usalama kazini

Singapore yaridhia mkataba wa ILO wa usalama kazini

Singapore imetia saini mkataba wa Shirika la Kazi Duniani ILO wa kuchagiza afya na usalama wa wafanyakazi kazini. Tangazo hilo limetolewa Jumatatu na waziri wa kazi na maendeleo ya nchi hiyo Tan Chuan-Jin wakati wa mkutano wa ILO unaoendelea mjini Geneva.

Amesema Singapore imekuwa ikijitahidi kuimarisha usalama wa wafanyakazi wake tangu kulipofanyika mabadiliko ya sheria ya afya na usalama kazini mwaka 2005.

Bwana Tan amesema hatua hizo zimesaidia kupunguza idadi ya vifo kutoka asilimia 4.5 kati ya watu 100,000 mwaka 2004 hadi kufikia asilimia 2.3 ya vifo kati ya watu 100,000 mwaka 2011.

(SAUTI TAN CHUAN-JIN)