Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa ILO ataka hatua zichukuliwe dhidi ya ajira kwa watoto

Mkuu wa ILO ataka hatua zichukuliwe dhidi ya ajira kwa watoto

Bado kuna pengo kubwa kati ya uridhiaji mkataba wa kupinga ajira kwa watoto na hatua za utekelezaji zinazochukliwa na nchi kukabiliana na tatizo hilo imesema ripoti ya shirika la kazi duniani ILO iliyotolewa kuadhimisha mwaka wa 10 wa sik ya kimataifa ya kupinga ajira ya watoto.

Kwa mjib wa mkurugenzi mkuu wa ILO Juan Somavia hakuna fursa ya kupoteza wakati watoto milioni 215 duniani bado wanafanyishwa kazi ili kishi na zaidi ya nusu ya watoto hao wako katika mifmo mibaya zaidi ya ajira, ikiwemo utumwa na kushirikishwa katika vita vya silaha.

Ameongeza kuwa dunia haiwezi kuruhus utokomezaji wa ajira ya watoto kurudisha nyma maendeleo, nchi zote lazima zijitahidi kufikia malengo. Alice Kariuki anaripoti.

(RIPOTI YA ALICE KARIUKI)