Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMA yashutumu vikali mashambulizi nchini Afghanistan

UNAMA yashutumu vikali mashambulizi nchini Afghanistan

Umoja wa Mataifa umekashifu vikali mashambulizi yaliyofanywa kwenye mikoa minne nchini Afghanistan ambayo yalisababisha vifo vya watu 40 wakiwemo watoto kumi na wengine 67 kujeruhiwa na kutaka wahusika kufikishwa mbele ya sheria.

Kulingana na ripoti za vyombo vya habari mashambulizi hayo ni pamoja na kujitoa mhanga yaliyoendeshwa na kundi la wanamgambo wa Taliban pamoja na mashambulizi ya anga yaliyoendeshwa na ndege za jumuiya ya kujihami ya nchi za magharibi NATO.

Kulingana na ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA ni kuwa mashambulizi ya kujitoa mhanga ndiyo yamewaua raia wengi zaidi nchini humo.