Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalam wa haki za binadam kuzuru Sudan

Mtaalam wa haki za binadam kuzuru Sudan

Mtaalam huru ambaye ameteuliwa na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya hali haki za binadam nchini Sudan, Mashood Adebayo Baderin, ataizuru Sudan tarehe 10-14 Juni, ili kuangalia sehemu zinazohitaji msaada wa kitaaluma na kuongeza uwezo wa taifa hilo wa kutekeleza majukumu yake ya kulinda haki za binadamu.

Kwenye ziara yake hiyo ya siku tano, Bwana Baderin atakutana na maafisa wa serikali, wawakilishi wa mashirika ya umma, mabalozi na mashirika ya Umoja wa Mataifa. Anatarajiwa kuwasilisha ripoti na mapendekezo yake mnamo mwezi Septemba mwaka huu, kwenye kikao cha 21 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa.