8 Juni 2012
Kumefanyika leo zoezi la kuendesha baiskeli kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, kama sehemu ya kuunga mkono juhudi na maudhui ya mkutano wa Rio+20, ambao unafanyika mjini Rio de Janeiro nchini Brazili mwezi huu.
Akizungumza kwenye hafla ya zoezi hilo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema kuwa desturi ya kuendesha baiskeli ni sehemu muhimu ya juhudi za kimataifa za kufikia maendeleo endeleveu.
(CLIP SAUTI YA BAN )