Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haki na usalama ni muhimu kwenye vita:UNDP

Haki na usalama ni muhimu kwenye vita:UNDP

Ripoti moja iliyotolewa na shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP,imeeleza kuwa kuwepo kwa hali ya usalama na utawala wa kisheria ni maeneo muhimu yanayoweza kutoa mustakabala mwema wa kurejesha hali ya utengamao kwenye maeneo yaliyokumbw a na mizozo.

Ripoti hiyo iliyochapishwa kwa mara ya kwanza New York inasema kuwa suala la usalama na uhakika wa maisha ndiyo mada muhimu inayozingatiwa na makundi yote ya watu hasa katika maeneo yaliyopitia mikwamo ya kisiasa.

Ikiwa na kichwa cha habari kisemacho uimarishaji wa utawala wa kisheria katika maeneo yaliyoathiriwa na mizozo ya kivita, ripoti hiyo imetoa takwimu zinazoenyesha nama tatazo la vita lililoathiri mataifa mengi.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kiasi cha watu bilioni 1.5 wanaendelea kuishi katika maeneo ambayo tayari yameonja adha za vita na mizozo.Ripoti pia imeelezea mafungamano yaliyopo baina ya maendeleo na suala la kuwalinda watu kutumbukia kwenye machafuko.