Ujenzi wa makazi ya Walowezi ni kinyume na sheria:Serry

7 Juni 2012

Mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya mpango wa amani wa Mashariki ya Kati, Robert Serry, ameongeza sauti yake kwa mtazamo wa jamii ya kimataifa kwamba, majengo yote katika maeneo ya makazi, yawe kwenye ardhi binafsi ya Palestina, au kwingineko kwenye maeneo yalokaliwa kwenye ardhi ya Palestina, ni kinyume na sheria za kimataifa.

Tangazo la hivi karibuni, pamoja na kuongeza kwa majengo mengine 300 kwenye eneo la Beit El ndani mwa Ukingo wa Magharibi, linasikitisha. Mratibu huyo maalum amerudia onyo allilotoa kwa Baraza la Usalama kuwa, ikiwa wanaohusika hawataitikia nafasi iliyopo sasa, watambue kuwa athari yake haitakuwa tu kupunguza kasi ya hatua zinazopigwa kufikia kuwepo mataifa mawili. Badala yake, zitakuwa hatua za kufikia kuwepo taifa moja tu, na hivyo kwenda hatua nyingi zaidi mbali na amani, kwa mujibu wa mpango wa amani wa jumuiya ya Kiarabu.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter