Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vyandarua vya bei nafu vitapunguza gharama:UNICEF

Vyandarua vya bei nafu vitapunguza gharama:UNICEF

Kupunguza bei ya vyandarua vya kuzuia mbu wanaosababisha malaria kunaweza kulisadia shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, kuokoa hadi dola milioni 22 za matumizi yake katika kipindi cha mwaka mmoja ujao, amesema leo mkuu wa shirika hilo.

 Wakati wa mkutano wa halmashauri ya UNICEF wa kila mwaka mjini New York, Mkurugenzi huyo mkuu wa UNICEF, Anthony Lake, amesema, wakati huu wa mdororo wa uchumi, uokoaji huu ni habari nzuri kwa serikali nyingi na nzuri hata zaidi kwa watoto. Jason Nyakundi anaripoti

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)