Ban aitaka jumuiya ya kimataifa kushikamana na kuchukua hatua pamoja dhidi ya Syria

Ban aitaka jumuiya ya kimataifa kushikamana na kuchukua hatua pamoja dhidi ya Syria

 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameitaka jumuiya ya kimataifa kushikamana na kuchuka hatua za pamoja katika saa na kipindi hii kigumu kwa Syria. Ban amesema hali ya Syria inaendelea kuzorota na kila siku mambo mapya yanazuka yanayoongeza zahma katika mauaji na uhalifu.

Akizungumza katika kikao maalumu cha Baraza Kuu Ban amesema mashambulizi dhidi ya raia, ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, kukamatwa kwa watu, utesaji, mauaji na kila upande kushindwa kushiriki mazungumzo kunafanya hali kuwa mbaya zaidi.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Kikao hicho ambacho kimehudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa jumuiya ya nchi za Kiarabu, mwakilishi wa Kamishina Mkuu wa Haki za Binadamu na mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za Kiarabu Syria Kofi Annan kinajaribu kupata suluhu mbadala ya kuleta amani Syria. Akizungumzia nini cha kufanya Kofi Annan amesema.

(SAUTI YA KOFI ANNAN)