Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bokova alaani mauaji ya mwandishi habari Pakistan

Bokova alaani mauaji ya mwandishi habari Pakistan

Mkurugenzi mkuu wa shirika la elimu sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO Irina Bokova amelaani mauaji ya mwandishi mmoja wa habari raia wa Pakistan na kutaka uchunguzi kufanywa.

Bokova amelaani mauji ya Abdul Qadir Hajizai yaliyofanyika eneo la Baluchistan na kuutaka utawala wa Pakistan kuwafikisha mbele ya sheria wahusika.

Ameongeza kuwa kuongezeka kwa visa vya kuuwa kwa waandhishi wa habari katika eneo hilo ni tisho kubwa kwa haki ya kupata habari suala ambalo amelitaja kuwa nguzo ya demokrasia.

Mwandishi huyo wa habari ambaye pia ni mwalimu wa shule moja alikuwa akifanya kazi na kituo kimoja cha runinga kinachotangaza kwa lugha ya Baluchi na alipigwa risasi na watu waliokuwa wakitumia pikipiki katika eneo la Basima kwenye mkoa wa Washik.