Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yaonya kuhusu aina ya Kisonono isiyo na tiba

WHO yaonya kuhusu aina ya Kisonono isiyo na tiba

Mamilioni ya watu wenye kisonono wanakabiliwa na hatari ya kukosa matibabu, kama hatua ya dharura haitochukuliwa, linasema shirika la Afya Duniani, WHO.

tayari, nchi kadhaa, zikiwemo Australia, Ufaransa, Japan, Norway, Sweden na Uingereza, zimeripoti visa vya dawa cephalosporin, ambayo ndiyo dawa ya mwisho yenye uwezo wa kutibu kisonono.

WHO inasema matumizi mabaya ya dawa ni mojawepo ya sababu kuu za kufanya dawa hizo kushindwa kuuponya. Dr. Manjoula Lutsi-Narasimhan kutoka WHO anasema, ikiwa ugonjwa wa kisonono hauwezi kutibiwa, athari zake ni kubwa kwani takriban watu milioni 106 wanaambukizwa kisonono kila mwaka, ugonjwa unaombukizwa kupitia vitendo vya ngono