Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yasaidia visima vya maji jimboni Abyei

IOM yasaidia visima vya maji jimboni Abyei

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM limefanikisha ukarabati wa visima kadhaa vya maji katika eneo la kaskazini mwa jimbo la Abyei kwa ajili ya kuwafikishia huduma za maji mamia ya wananchi kwenye eneo hilo wenye asili ya kuhama hama.

Watu hao wa jamii ya Misseriya pamoja na mifugo yao, wanarejea katika eneo la kaskazini wakitokea katika jimbo la moja lililoko Sudan Kusin.

Kwa mara kadhaa kumeripotiwa hali ya mitafaruko baina ya wafugaji hao na jamii ya wakulima katika kile kinachoelezwa mzozo wa kugombea ardhi.

Kuwasili kwa kundi hilo la watu kwenye eneo hilo kunaweza kukasababisha hali ya sintofahamu na kurejesha mkwamo mpya wa ardhi kutokana na udogo wa eneo la ulishishaji mifugo.

Visima hivyo vya maji viliandaliwa vinauweza wa kuwahudumia zaidi ya watu 14,000 huku pia vikichukua nafasi ya kuwahudumia jamii ya wahamiaji wanaokadiriwa kufikia 200,000 pamoja na mifugo yao.