Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ataka mataifa kuongeza nguvu kukabiliana na vitendo vya kigaidi

Ban ataka mataifa kuongeza nguvu kukabiliana na vitendo vya kigaidi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameyatolea mwito mataifa duniani kongeza kasi ya kukabiliana na wimbi la vitendo vya kigaidi huku akitaja vipaumbele kadhaa vinavyoweza kuchagiza ushindi juu ya kadhia hiyo.

 Akizungumza kwenye mkutano wa bodi ya washauri juu ya kukabiliana na vitendo hivyo vya ugaidi huko Jeddah Saudia Arabia, Ban amesema kuwa hakuna taifa linaloweza kujivuna kuwa salama na mashambulizi ya kigaidi, hivyo kutokana na hali hiyo kunapaswa kuwa na mashirikiano ya dhati kukabili hujuma hizo.

Ban pamoja na kusifu hatua zinazoendelea kuchukuliwa na mataifa kukabiliana na vitendo hivyo lakini hata hivyo amehimiza kuibuliwa na nguvu za pamoja tena katika wakati muafaka kwani kitisho kilichopo mbele bado ni kikubwa.

 Bado hiyo ya washauri ya Umoja wa Mataifa UNCCT ilianzishwa rasmi Septemba 2010 kwa msaada mkubwa wa serikali ya Saudia Arabia ikiwa na lengo la kusuma mbele shughuli za kukabiliana na matukio ya ugaidi kote duniani.