Ugaidi unaendelea kuathiri maeneo yote duniani:Ban

4 Juni 2012

 

Kuna haja ya haraka ya kukabiliana na ugaidi, kwani ugaidi unaendelea kuathiri maeneo yote duniani, na umeharibu maisha ya mamilioni ya watu na kufuta matumaini ya amani na maendeleo amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.

Akizungumza Jumapili kwenye mkutano wa pili wa bodi ya shauri wa kituo cha Umoja wa Mataifa cha kupambana na ugaidi mjini Jeddah Saudia Ban amesema licha ya machungu na athari zote dunia inakabiliana na uhalifu huu.

Mkakati wa Umoja wa ataifa wa kupambana na ugaidi duniani uuliopitishwa bila kupingwa na wajumbe wote kwenye Baraza Kuu ni kiungo kikubwa cha juhudi za kimataifa kupambana na ugaidi. Ban amesema kimikakati dunia inahitaji kujaribu kuelewa na kupinga ugaidi, hii ikimaanisha kujenga utamaduuni wa kjadili sala hili, kuelimisha na kuchagiza mahusiano ya kijamii.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter