Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serikali ya Burundi yaanza kampeni dhidi ya Polio

Serikali ya Burundi yaanza kampeni dhidi ya Polio

Serikali ya Burundi kwa ushirikiano na shirika la Afya Duniani WHO wameanzisha kampeni kabambe dhidi ya ugonjwa wa polio. Hii ni baada ya Burundi kujikuta katika kitisho kikubwa cha kuvamiwa na maradhi hayo baada ya nchi jirani ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuonyesha dalili za Polio katika maeneo ya kusini na mashariki mwa nchi hiyo.

Watoto zaidi ya Milioni 1 na Laki 2 wanahusishwa na kampeni hii ambayo pia Shirika la WHO limepania kuineza katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kutoka Bujumbura, Muandishi wetu wa Maziwa Makuu Ramadhani KIBUGA anafuatilia zoezi hilo la chanjo na ametuandalia makala hii.

(MAKALA YA RAMADHANI KIBUGA)