Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Haki za Binadamu la UM lafanya kikao kujadili hali nchini Syria

Baraza la Haki za Binadamu la UM lafanya kikao kujadili hali nchini Syria

Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa linafanya kikao cha dharura cha kujadili mzozo na kuendelea kuzorota kwa hali ya kibinadamu nchini Syria. Kikao hicho kinatarajiwa kuangazia kisa cha hivi karibuni cha mauaji ya raia 108 wakiwemo watoto 49 na wanawake 34 kwenye kijiji cha EL-Houle mauaji ambayo yanakisiwa kutekelewa na makundi ya waasi.

Kwenye ujumbe kwa baraza hilo Kamishina Kkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay hata hivyo anasema kuwa kuna ushahidi kuwa mauaji hayo yalitekelezwa na wanajeshi wa Syria. Pillay amesema kuwa serikali ya Syria ni lazima ichukue jukumu la kuwalinda wananchi wake akiongeza kuwa wale wanaoshindwa kuwalinda raia kutokana na vitendo kama hivyo pia nao ni wahalifu. Marcia Kran alisoma ujumbe wa Kamishna Mkuu Navi Pillay.