Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Moldova ni lazima itekeleze Sheria zinazoua Ubaguzi wa Kijinsia:UM

Moldova ni lazima itekeleze Sheria zinazoua Ubaguzi wa Kijinsia:UM

Kundi la wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa wameitaka serikali ya Moldova kutekeleza sheria inayokataa ubaguzi kama moja ya njia ya kuzuia ubaguzi wa kijinsia na kulinda haki za wanawake. Kundi hilo lilikuwa nchini Moldova kwa muda wa siku kumi ambapo lilikutana na maafisa wa serikali, wawakilishi wa idara ya mahakama, mashirika ya umma, dini mbali mbali pamoja na jamii ya wanawake. Wataalamu hao walisisitiza kuwa kuna mwanya mkubwa kati ya sheria na kutekelezwa kwake hasa kwenye dhuluma za nyumbani na usafirishaji haramu wa watu.

Mkuu wa kundi la Umoja wa Mataifa linalopinga ubaguzi dhidi ya wanawake Kamala Chandrakirama amesema kuwa hatua zinahitaji kuchukliwa kuhakikisha kuwa wanawake wanashiriki katika kutoa maamuzi kwenye nyanja zote.