31 Mei 2012
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha kuondoka kabisa kwa vikosi vya Sudan Kusini kutoka eneo linalozozaniwa la Abyei. Kupitia kwa msemaji wake Ban amezitaka serikali za Sudan na Sudan Kusini mara moja kubuni usimamizi wa eneo hilo ambao itawahakikishia amani wenyeji wake chini ya makubalino ya tarehe 20 mwezi Juni mwaka uliopita . Sudan Kusini ilipata uhuru wake kutoka Sudan mwezi Julai mwaka uliopita miaka sita baada ya kusainiwa kwa kubaliano yaliyomaliza miongo kadha ya vita kati ya eneo la kusini na Kaskazini.
Hata hivyo usalama kati ya mataifa hayo umekuwa ukivurugwa na mapigano kwenye mpaka kati ya mataifa hayo na mizozo kuhusu umiliki wa maeneo fulani.