Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UNESCO alaani Mauwaji ya Mwandishi Somalia

Mkuu wa UNESCO alaani Mauwaji ya Mwandishi Somalia

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalojihusisha na masula ya elimu, sayansi na utamaduni UNESCO amelaani vikali tukio la kuuliwa kwa mwandishi wa habari wa Somalia na ameitolea mwito mamlaka nchini humo wahusika wa tukio hilo wanaletwa kwenye mkono wa dola.

Mwandishi huyo wa habari Ahmed Addow Anshur alikuwa akifanya kazi na kituo cha redio Shabelle aliuwawa na watu wasiojulikana mjini Mogadishu hapo May 24.

Akilaani tukio hilo, Mkurugenzi wa UNESCO shirika linalohusika pia na utetezi wa uhuru wa kujieleza, Bi Irina Bokova amesema kuwa kuendelea kuachia mwenendo wa mauwaji kwa waandishi wa habari ni hatari kwa mustakabali wa taalumu ya uandishi wa habari.

Kumekuwa na ripoti za mara kwa mara zinahusu kuuliwa kwa waandishi wa habari wakiwa kwenye shughuli zao.