Matumizi ya Silaha siyo Suluhu ya Kumaliza Tatizo Syria

31 Mei 2012

Afisa mmoja kutoka Umoja wa Mataifa amesema kuwa kuendelea kushadidi kwa matumizi ya silaha katika maeneo yanayokabiliwa na mikwamo nchini Syria, hakuwezi kutoa suluhu badala yake ni kuangamiza eneo hilo.

Akionya juu ya hatari inayosalia mbele kwa Syria, Naibu Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya kiarabu Jean-Marie Guéhenno, amesema kuwa msururu wa matumizi ya silaha za kijeshi ni hatari tena inaweza kuleta maafa makubwa kwa taifa hilo.

Ameeleza kusema kuwa baada ya kipindi cha mashambulizi cha zaidi ya miezi 15 sasa, suala linasalia kumaliza mkwamo huo ni kuanzisha ishara zenye nguzu na ushawishi mkali.

Mtaalamu huyo amesema kuwa utashi wa kisiasa unahitajika sasa ili kufanikisha majadiliano ya umalizaji mapigano.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter