Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yahofia raia wa Syria walioko Kaskazini mwa Iraq

UNHCR yahofia raia wa Syria walioko Kaskazini mwa Iraq

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, limeelezea wasiwasi wake kuhusu ongezeko la idadi ya raia wa Syria wanaokimbilia kaskazini mwa Iraq. Kufikia tarere 30 Mei, takriban watu alfu nne na mia nne raia wa Syria wenye asili ya KiKurdi walikuwa wameandikishwa na, UNHCR na idara ya uhamiaji, (DDM).

Takriban jamaa 10 au watu 100 hadi 200 binafsi wanaendelea kuingia eneo la Duhok Govenrorate kila wiki, kuashiria ongezeko la watu kutoka Syria. Viongozi wa mikoani wanasema idadi ya watu waliojiandikisha haiashirii idadi kamili ya raia wa Syria wanaowasili katika eneo hilo, ambayo wanakisia kuwa 6, 000.