Watu milioni 8 Watakufa kila mwaka ifikapo 2030 kutokana na Athari za Tumbaku:WHO

31 Mei 2012

Tumbaku inauwa takribani nusu ya watumiaji wake, kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO ambalo linafanya kazi kila siku kuwalinda watu kutokana na athari za bidhaa za tumbaku ambazo kwa sasa huuwa watu milioni 6 kila mwaka.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva katika siku hii ya kimataifa ya kupinga matumizi ya tumbaku mkurugenzi wa mradi wa WHO wa kuwa huru na tumbaku Douglas Bettcher amesema ifikapo mwaka 2030 WHO inakadiria kwamba tumbaku itakatili maisha ya watu milioni 8 kila mwaka, huku vifo vine kati ya vitano vikitokea katika nchi za kipato cha chini na cha wastani.

Tumbaku imetajwa kuwa ni chachu kubwa ya maradhi yasiyo ya kuambukiza kama saratani, magonjwa ya moyo, kisukari na matatizo ya kupumua. Na magonjwa haya yanachangia asilimia 63 ya vifo vyote duniani. Mwandishi wetu wa Burundi Kibuga Ramadhani amezungumza na baadhi ya wananchi kupata maoani yao kuhusu matumizi ya tumbaku.

(MAONI BURUNDI SIGARA)

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter