Mkuu wa UM aonya kuhusu Vita vya Wenyewe kwa Wenyewe Syria

31 Mei 2012

Mauaji ya watu kama yaliyoshuhudiwa wiki iliyopita yanaweza kuitumbukiza Syria katika vita vikubwa vya wenyewe kwa wenyewe, vita ambavyo taifa hilo halitoweza kamwe kupona ameonya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.

Ban ametoa onyo hilo kwenye fuunguzi wa kongamano la Umoja wa Mataifa la muungano wa ustaarabu lililoanza Alhamisi mjini Instanbul Uturuki. Ban amesema anaitaka serikali ya Syria kuchukua hatua za kutimiza wajibu wake chini ya mpango wa amani wa Kofi Annan. Ameongeza kuwa jumuiya ya kimataifa inaitaka serikali ya Syria kutimiza jukumu kwa watu wake, kwani ameweka bayana kwamba mpango wa Umoja wa Mataifa haujapelekwa Syria kushuhudia mauaji ya watu wasio na hatia, wala kuangalia uhalifu usiokubalika.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter