Zaidi ya dola Milioni 427 zilizotolewa kusaidia Huduma za Kibinadamu mwaka uliopita

30 Mei 2012

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa ilitoa misaada ya dharura wa zaidi ya dola milioni 427 mwaka uliopita kusaidia nchi zilizoathiriwa na majanga kama vile ukame, mafuriko na usalama wa chakula.

Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2011 inayoonyesha mchango wa mfuko wa huduma za dharura wa Umoja wa Mataifa CERF kwa nchi 45. Mfuko huu unafadhiliwa na nchi wanachama , mashirika yasiyokuwa ya kiserikali , sekta za kibinafsi na ulibuniwa na Umoja wa Mataifa kwa lengo la kuhakikisha kuwepo kwa misaada ya kibinadamu wakati kunapotokea majanga ya kiasili na mizozo.

Kulingana na shirika la kuratibu masusla ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA ni kwamban majanga yanayohusiana na hali ya hewa yanayosabishwa na ukame na mafuriko yalipokea dola milioni 149 kutoka CERF.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter