Mradi wa Uingereza wa Uchunguzi dhidi ya Ubakaji ni muhimu:Wahlstrom

30 Mei 2012

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili wa kimapenzi katika maeneo ya vita Margot Wallstrom amekaribisha tangazo la serikali ya Uingereza la kuunda haraka kitengo maalum cha kukusanya ushahidi wa vitendo vya ukatili wa kingono uliotekelezwa katika maeneo ya vita.

Bi Wallstrom pia amekaribisha tangazo la nchi hiyo lenye lengo la ktmia nafasi yake kama Rais wa G-8 mwakani kchagiza kuhusu sala hilo la ukatili wa kimapenzi. Katika taarifa yake Bi Wallstrom amesema kufungua mashitaka dhidi ya ukatili wa kimapenzi pia ni njia ya kuuzia, kwani itakwa inatuma ujumbe kwa wahusika kwamba kukwepa mkono wa sheria sio chaguo hasa kwa halifu kama ho.

Na amesema ushahidi wowote utakaokusanywa utasaidia kuwafungulia kesi wahusika na kimarisha juhudi za pamoja za kukabiliana na uhalifu kama ubakaji.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter