Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mfanyakazi wa WFP aachiliwa Huru Darfur baada ya Siku 80

Mfanyakazi wa WFP aachiliwa Huru Darfur baada ya Siku 80

Siku 80 baada ya kutekwa nyara, kusini mwa eneo la Sudan la Darfur, mfanyikazi wa huduma za kibinadamu raia wa Uingereza, Patrick Noonan Sudan, ameachiliwa huru. Bwana Noonan alikuwa akifanya kazi ni Shirika la Utoaji Msaada wa chakula la Umoja wa Mataifa, WFP.

Mkurugenzi Mkuu wa WFP, Ertharin Cousin ameelezea furaha ya wafanyikazi wenzie wa WFP, akisema Bwana Noonan alikwenda Darfur kwa lengo la kuwasaidia watu wanyonge, na kutekwa kwake nyara kumekuwa mzigo sana kwa jamaa, wafanyikazi wenzie na marafiki.

Noonan ambaye alikuwa akifanya kazi kama msimamizi wa vifaa na shughuli za huduma, alitekwa nyara tarehe sita Mwezi Machi mwaka 2012, pamoja na dreva raia wa Sudan ambaye aliachiliwa siku hiyo hiyo.