Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hakuna Maendeleo Endelevu bila Kutokomeza Njaa

Hakuna Maendeleo Endelevu bila Kutokomeza Njaa

Maendeleo endelevu hayawezi kupatikana hadi pale njaa na utapia mlo utakapotokomezwa imesema taarifa ya shirika la chakula na kilimo FAO iliyoandaliwa kwa ajili ya mkutano wa Rio+20 unaotarajiwa kufanyika Juni Rio de Janeiro .

Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa FAO Jose Graziano da Silva maendeleo hayawezi kuitwa endelevu wakati hali inazidi kuwa mbaya na huku karibu kila mtu mmoja kati ya saba wanaume wanawake na watoto wamesalia nyuma na hawana lishe bora.

Ameongeza kuwa suala la usalama wa chakula linaweza kuwa daraja la kuunganisha changamoto tofauti zinazoikabili dunia na kusaidia kuboresha mustakhbali wa baadaye wa maisha ya watu. Amesema kwenye mkutano wa Rio ni fursa ya kipekee ya kutafakari ajenda za usalama wa chakula na maendeleo endelevu na kuhakikisha vinakwenda sambamba.