Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya Haki za Binadamu Iraq Bado ni Tete:Ripoti ya UM

Hali ya Haki za Binadamu Iraq Bado ni Tete:Ripoti ya UM

Hali ya haki za binadamu nchini Iraq bado ni tete, wakati taifa hilo linaendelea kujikwamua kutoka kwa uongozi wa kiimla, mizozo na ghasia na kuingia amani na demokrasia. Hii ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Iraq kwa mwaka 2011.

Ripoti za mara kwa mara kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Iraq, huchapishwa na Idara ya Umoja wa Mataifa ya Kutoa Msaada Iraq, yaani UNAMI, ikishirikiana na Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu, kufuatia azimio namba 1770, ambalio lilianzisha UNAMI, pamoja na maazimio mengine ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA )