Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mahakama ya Rufaa ya ICC yasema Mbarushimana hastahili Kushtakiwa

Mahakama ya Rufaa ya ICC yasema Mbarushimana hastahili Kushtakiwa

Mahakama ya rufaa ya ICC, leo imekataa na kutupilia mbali ombi la upande wa mashtaka dhidi ya uamuzi wa jopo la majaji la kwanza, ambalo lilikataa kuthibitisha mashtaka dhidi ya Bwana Callixte Mbarushimana.

Jaji Erkki Kourula, ambaye amesimamia rufaa hii, ametangaza uamuzi huo kwa kifupi katika kikao cha hadhara. Ameeleza kuwa Jopo la Rufaa lilikataa sababu mbili za kwanza za ombi la upande wa mashtaka, linalohusiana na uwezo wa jopo la kwanza wa kutathmini ushahidi kwenye hatua ya kuthibitisha mashtaka. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)