Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makampuni ya Sigara yahujumu Kampeni dhidi ya Matumizi ya Tumbaku:WHO

Makampuni ya Sigara yahujumu Kampeni dhidi ya Matumizi ya Tumbaku:WHO

Makampuni ya tumbaku yanatumia hela na mbinu chafu kudhoofisha vita dhidi ya matumizi ya tumbaku limesema shirika la afya duniani WHO. Mbinu hizo ni pamoja na kuchagiza mlolongo wa hatua za kisheria dhidi ya serikali ambazo zimekuwa msitari wa mbele kwenye vita dhidi ya bidhaa za tumbaku, kuongeza chumvi kuhusu umuhimu wa kiuchumi wa bidhaa za tumbaku na kutotilia maanani thibitisho la kisayansi la madhara ya kiafya yatokanayo na matumizi ya tumbaku.

Ikiwa ni katika maandalizi ya siku ya kimataifa ya kupinga matumizi ya tumbaku ambayo huadhimishwa Mai 31, WHO imezitaka serikali kuwa makini kutokana na ongezeko la mashambulizi ya makampuni ya tumbaku Dr Douglas Bettcher ni mkurugenzi wa idara ya WHO ya mradi wa kuachana na tumbaku.

(SAUTI YA DR DOUGLAS BETTCHER)

WHO inasema tumbaku inauwa takribani watu milioni 6 kila mwaka na ni moja ya vyanzo vya maradhi na vifo vinavyoweza kuzuilika duniani.