Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kofi Annan Azuru Syria na Kuelezea Hali ya sasa kuwa ni Tete

Kofi Annan Azuru Syria na Kuelezea Hali ya sasa kuwa ni Tete

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya nchi za kiarabu Kofi Annan amewasili katika mji mkuu wa Syria na kuelezea hali jumla ya mambo nchini humo ni tete ikiwa ni siku moja tu kulipotolewa ripoti ya kuuliwa kwa watu kadhaa.

Ziara ya Annan huko Damascus inakuja katika kipindi kukiarifiwa kuwepo kwa mauwaji ya raia zaidi ya 100 ikiwemo watoto 30 wengi wao wakiwa na umri wa chini ya miaka 10 mauwaji yaliyofanyika katika kijiji cha Houla siku mbili zilizopita.

Waangalizi kutoka ujumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Syria UNSIMS ambao ulitembelea eneo hilo mwishoni mwa juma umedhibitisha kuwepo kwa mauji hayo na matumizi ya silaha nzito katika makazi ya watu wanaozunguka eneo hilo.

Akizungumza baada ya kuwasili nchini humo Annan pamoja na kulaani mauwaji hayo lakini ameelezea masikitiko yake akisema kuwa kitendo hicho kinaogopesha na kutisha.