Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yaanza Kuwasaidia Mamia ya Waliokosa Makazi Mogadishu

UNHCR yaanza Kuwasaidia Mamia ya Waliokosa Makazi Mogadishu

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limeanza kufanya kazi kwa kushirikiana na wahisani wengine kuwapa msaada wa dharula kwa mamia ya watu waliokosa makazi wanaowasili mjini Mogadishu wakitokea eneo la Afgooye..

Tangu tarehe 22 mwezi May inakadiriwa kiasi cha watu 14,000 wamekosa makazi kutokana na mwingiliano wa shughuli za kijeshi zilizoanzishwa kwenye eneo hilo.

Pamoja na kukabiliwa na mkwamo wa ukosefu wa makazi wanachi hao kadhalika wanaandamwa na majanga mengine ya kibinadamu.

Makundi ya watu hata hivyo yanaendelea kulikimbia eneo hilo na wengine kadhaa wanaripotiwa kuwasili huko Shabelle na Juba China.