Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNRWA na Australia zasaini Mkataba wa dola milioni 90

UNRWA na Australia zasaini Mkataba wa dola milioni 90

Serikali ya Australia imetia saini ya ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA, katika kuchangia miradi ya UNRWA katika eneo zima la Mashariki ya Kati katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Takriban dola milioni 90 za kimarekani zitatolewa kwa ajili ya kuigharimia miradi hiyo, kwa mujibu wa mkataba huo wa ushirikiano, ambao umesainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Australia, Bob Carr na Kamishna Mkuu wa UNRWA, Filipo Grandi.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kutia mktaba saini, Bwana Grandi ameipongeza Australia na kuilelezea kama mfano wa mfadhili anayeongeza mchango wake wa muda mrefu kwa UNRWA katika njia endelevu na inayotegemewa.