Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM Kuongeza Makao Zaidi kwa Waathiriwa wa Mafuriko nchini Pakistan

IOM Kuongeza Makao Zaidi kwa Waathiriwa wa Mafuriko nchini Pakistan

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linatarajiwa kuongeza nyumba za chumba kimoja kutoka nyumba 10,500 hadi nyumba 30,000 zitakazokuwa makao kwa familia zilizoachwa bila makao kutokana na mafuriko yaliyoukumba mkoa wa Sindh nchini Pakistan mwaka 2011.

Mpango huo unaotoa fedha na usaidizi wa kiufundi kwa familia zilizoachwa bila makao kujenga upya unatarajiwa kuwafikia watu 75,000 ifikapo mwezi Mei mwaka 2013 na hadi watu 210,000 ikiwa utafadhiliwa. Mpango huo ulionzishwa mwaka huu mkoani Sindh tayari umetambua familia 3,300 zinazohitaji misaada au watu 21,000 ambao nyumba zao ziliharibiwa kabisa na mafuriko yaliyoukumba mkoa wa Sindh mwezi Agosti na Septemba mwaka uliopita na kuwaathiri watu milioni 5.8.