Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano yawalazimu zaidi ya 40,000 kuhama Makwao nchini DRC

Mapigano yawalazimu zaidi ya 40,000 kuhama Makwao nchini DRC

Idadi ya watu wanaokimbia mapigano kwenye Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na kuingia Rwanda na Burundi inaripotiwa kupungua baada ya mapigano kuwalizimu kiasi kikubwa cha watu kuhama makwao kwenye mkoa wa kivu kaskazini.

Wafanyikazi wa shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa mkoani kivu kaskazini wanasema kuwa idai kubwa ya watu wanalihama eneo la Rutshuru lililo kaskazni mwa mji wa Goma. Hadi sasa zaidi ya watu 40,000 wanaripotiwa kuhama makwao huku mapigano zaidi yakiripotiwa kwenye eneo la Runyonyi kati ya vikosi vya serikali na wanajeshi waasi waaminifu kwa kamanda wa zamani Basco Ntaganda mwishoni mwa juma.

UNHCR na mashirika mengine likiwemo shirika la mpango wa chakula duniani WFP, shirika la afya duniani WHO na kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu wana mipango ya kuanzisha usambazaji wa chakula , madawa na misaada mingine kwa watu waliohama makwao. Mellissa Flemming ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA MELISSA FLEMMING)