Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni Lazima Ghasia Zikomeshwe na Mpango wa Amani Kutekelezwa Syria:Kofi Annan

Ni Lazima Ghasia Zikomeshwe na Mpango wa Amani Kutekelezwa Syria:Kofi Annan

Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za Kiarabu, Kofi Annan, amekutana na Rais Bashar-al-Assad leo kuelezea kusikitishwa kwa jamii ya kimataifa na ghasia nchini Syria, na hasa matukio ya hivi karibuni kwenye kijiji cha Houleh karibu na mji wa Homs.

Bwana Annan amemwelezea rais Assad kuwa mpango ulowekwa wa hatua sita hauwezi kufanikiwa bila kuwepo hatua mathubuti za kukomesha ghasia na kuwaachilia huru mateka. Bwana Annan pia amesisitiza umuhimu wa kuutekeleza kikamilifu mpango ulokubaliwa wa hatua sita.