Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mbinu Mpya ya Huduma za Afya yaleta afueni kwa Wakimbizi wa Kipalestina:UNRWA

Mbinu Mpya ya Huduma za Afya yaleta afueni kwa Wakimbizi wa Kipalestina:UNRWA

Shirika la Umoja wa Mataifa la Msaada kwa ajili wa Wakimbizi wa Kipalestina, UNRWA, limeanzisha mbinu mpya ya kutoa huduma za afya, ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa afya na maisha ya mamia ya maelfu ya wakimbizi hao. Mbinu hiyo inayolenga familia moja kwa moja, inakabiliana na maswala ya afya, hasa yanayohusiana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza, kama vile kisukari na msukumo wa damu, kwa kuzihusisha jamii katika kubadili desturi za maisha. Mbinu hii iloanzia katika vituo viwili vya afya kama jaribio mwaka 2011, inatilia maanani inahusisha jamii nzima katika maswala ya afya na kuwahudumia wagonjwa, na sasa imepata sifa kutoka kwa wale walionufaika nayo.