Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akaribisha hatua ya Sudan mbili kukubali kurejea kwenye meza ya majadiliano

Ban akaribisha hatua ya Sudan mbili kukubali kurejea kwenye meza ya majadiliano

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha na kupongeza hatua ya Sudan mbili kukubali kurejea kwenye meza ya majadiliano kwa shabaha ya kutanzua mzozo unaoliandama eneo hilo.

Mataifa hayo Sudan na Sudan Kusin yamekubaliana kukutana tena wiki ijayo mjini Addis Ababa yakiwa na matumaini kufikia suluhu kwenye mzozo wao kuhusiana na umiliki wa eneo lenye utajiri mkubwa wa mafuta.

Ban pamoja na kupongeza hatua hiyo ya kujongeleana tena, lakini amezitaka pande zote kuonyesha utashi wa kufikiana makubaliano ambayo yatafanikisha kufikiwa kwa suluhu ya kudumu..

Mzozo wa pande hizo inakuja kufuatia hatua ya Sudan Kusin kuwa taifa kamili mwezi July mwaka uliopita 2011. Kuzaliwa kwa taifa hilo jipya na utekelezwaji wa makubaliano ya usitishwaji mapigano yaliyodumu kwa miongo kadhaa na kuzorotesha ustawi wa eneo hilo.