Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yafungua ofisi nyingine kuwasaidia Wakimbizi wa Dadaab

UNHCR yafungua ofisi nyingine kuwasaidia Wakimbizi wa Dadaab

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi UNHCR limefungua ofisi yake nyingine katika kambi ya Dadaab iliyopo kaskazini mashariki mwa Kenya, ikiwa ni sehemu ya kuumarisha shughuli za utoaji wa huduma.

Kambi hiyo inayokadiriwa kuchukua wakimbizi zaidi ya 460,000 inatajwa kuwa kambi yenye kuchukua idadi kubwa ya wakimbizi.

UNHCR ilianzisha ofisi yake kwenye eneo hilo ikilenga kuimarisha huduma za kuwakirimu wakimbizi hao ambao wanakabiliwa pia na changamoto kadhaa.

Kambi hiyo inayojulikana kwa jina la Alinjugur ipo katika jimbo la Fafi ambalo lina umbali wa kilometa 80 toka mpakani mwa Somalia