Hali ya Kibinadamu yazidi kuwa mbaya nchini DRC:ICRC

25 Mei 2012

Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu ICRC inasema kuwa bado ghasia zinaendeea kushuhudiwa kwenye mikoa ya kivu kwenye Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. ICRC ina wasiwasi kuhusu idadi ya raia wanaoendelea kuathiriwa na ghasia hizo ambapo imetoa wito kwa pande husika kuyajali maisha ya raia. Inasema kuwa wanaoathiriwa zaidi ni watoto, watu wazee na akina mama . Mapigano hayo ambayo yameshuhudiwa kwenye maeneo ya Walungu, Shabunda na Kalehe ya mkoa wa Kivu kusini yamewalazimu wenyeji kukimbia makwao mapigano ambayo pia yamesabaisha vifo na majeraha mengi hasa kwenye sehemu za Walikale na Masisi mkoani Kivu Kaskazini.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud